Licha ya kwamba sehemu kubwa ya Hifadhi ya Serengeti ni uwanda wa nyasi, ndani ya hifadhi hii pia kuna mito na mabwawa kadhaa ambayo yamejaa viboko na mamba wa kutosha. Lipo la Retima (retima hippo pool) na hili ni mojawapo ambalo lipo ktk mto Seronera unaokatisha katikati ya hifadhi. Bwawa hili lipo ktk usawa wa moja ya routes ambazo hot air balloons zinapita. Abiria wa balloons hupata fursa (endapo Baloon yenu itapita juu ya hili bwawa au karibu) kuwaona hawa jamaa tokea juu.
Picha hizi zilipigwa tokea ktk hot Air balloon inayomilikiwa na Serengeti Ballon safaris ambayo hufanya safari zake ndani ya hifadhi ya Serengeti
Yap!!!, yani umenirudisha home enzi zangu nilipo kuwa ninafanya kazi ya Tour Guide pale Migration Camp Serengeti mwaka 2008,yani ungenionyesha wa chini na kisukuma mavi ninge furahi sana. Hivi sasa nipo hapa Italy nasoma hii lugha ya watu mashap(duka) na mkono wa birika.
ReplyDeleteSalam kwa waongoza watalii wote hapo nyumbani Tz,nipo pamoja nanyi.
Conf.