Thursday, February 18, 2010

Pimbi

Hapo zamani kidogo kulikuwepo na jarida moja likijulikana kama Gazeti la Sani - natumai bado lipo kwani siku hizi yamekuwa mengi mno. Ndani ya jarida hilo kulikuwa na characters kadhaa, mmoja wao ambae alikuwa haishi kukumbwa na misukosuko ktk issue zake alijulikana kama Pimbi aka Dr. Love. Jamaa alikuwa na nuksi kama analala na bundi vile, maana issue zake zilikuwa zinatibuka dakika za majeruhi.
Picha juu ndio mnyama mwenyewe pimbi kama alivyofumwa na team ya TembeaTz ndani ya Serengeti Np.

Ndani ya Serengeti NP kuna sehemu maalum ya wageni kwenda kupata taarifa mbalimbali kuhusu Serengeti NP. inaitwa information Center. Ukifika sehemu hii, utawakuta pimbi wa kumwaga. wanatembea huru na hawaogopi watu.

No comments:

Post a Comment