Wednesday, December 30, 2009

Toli toli za Mlima Kilimanjaro

Ikitokea mpanda mlima kachemsha kiasi cha kushindwa kujimudu, basi uzionazo hapo chini ya hilo banda ndio ambulance zinazotumika kumshusha mpandaji hadi getini ili kupata huduma zaidi. Hali ya kuchemsha hutokea endapo mgeni atashindwa kumudu mikiki ya hali ya hewa ya mlimani yenye upungufu wa hewa ya oksijeni. U
kitaka kukwea vyema mlima Kilimanjaro mazoezi ni muhimu na pia unatakiwa kufuata masharti unayoelekezwa na guide wako. kwa kifupi, ukiwa unapanda mlima unatakiwa kufanya mambo makuu yafuatayo; Kula, Kulala na Kutembea; K-tatu. Fanya haya kufuatana na maelekezo ya guide - usizidishe na wala usipunguze. ukifuata ushauri wao, utafanikiwa kufika kileleni.

Ahsante ya picha kwa wadau - Friendz of TembeaTz - walioamua kusherehekea X-mass ya mwaka huu kwa kuukwea mlima. Pongezi kwenu wadau kwa kudumisha dhana ya utalii wa ndani. Stei tyund kwa picha zaidi za safari ya friends of TembeaTz huko Mlima Kilimanjaro

1 comment:

  1. Hizi tol tol za mlima kilimanjaro wengine wanaziita (Machela) kwa kweli kama umechoka usidanganye kuwa unaumwa ii wakubebe na hiyo toli toli. Wanaikimbiza inadunda dunda kama kitenesi na ukizingatia wakati huo huwa ni mreremko na wamekufunga mikanda, kweli utaipata.

    ReplyDelete