Wednesday, December 30, 2009

Mambo ya Ngorongoro

Picha ni gate la kuingilia Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) likiwa lina meremeta baada ya kupigwa face lift ya nguvu. Pongezi kwa NCAA kwa juhudi za kuhakikisha kuwa Ngorongoro crater inavutia kila nyanja. Squad ya TembeTz ilipita gateni hapo mwishoni mwa mwezi April 2009 na kukuta ujenzi huu ukiwa ktk hatua za mwanzo.
Hivi ndivyo gate lilivyo sasa, inapendeza, inavutia na inahamasisha.
Shime wadau tutembelee vivutio vyetu ili tujionee Tanzania yetu ilivyobarikiwa na mandhari maridhawa zenye kuliwaza na kupumzisha akili yako pindi uwapo huko.

Unapofika ktk gate la kuingilia NCAA, hakikisha kuwa vioo vya gari na roof ya gari (kama ni safari vehicle) zimefungwa. Hawa jamaa ndio mateja wa eneo hilo. Kwa uelewa na uzoefu wao, Hawa jamaa wanajua kuwa magari yanayoingia ktk NCAA huwa yanakuwa na lunch box, hivyo hawa jamaa timing yao ni kwenye kitu chochote kilichofungwa ambacho watakikuta ndani ya gari lako. ikitokea wanaifuma lunch box yako, basi jua siku hiyo utafanya game drive bila lunch au itakubidi ujongee hotel mojawapo ukapate mlo wa mchana. hawaachi kitu.
Pia usithubute kula chakula hapo, uta share nao bila kupenda.

Moja ya mambo ambayo UNESCO inatumia kama kigezo cha kutishia kuiondoa NCAA ktk list ya world heritage site ni uwepo wa makazi ya watu na mifugo (Ngombe na Mbuzi) ndani ya eneo la hifadhi. kwa taratibu za UNESCO, eneo la hifadhi ni enao ambalo halipashwi kutumika kwa makazi.
Picha juu ni moja ya Boma za wamasai zilizo nje ya crater, lakini ndani ya enao la NCAA ambapo wageni hutembelea na kupata taarifa mbalimbali za maisha ya jamii ya wamasai.

Ahsante ya picha kwa mdau kupitia kwa Ankal

No comments:

Post a Comment