Tuesday, December 29, 2009

Naabi Hill - Serengeti

Kama utaingia hifadhi ya Serengeti (kwa barabara) ukitokea Ngorongoro, basi huwezi kukosa kupita hapa - Naabi Hill. Naabi Hill ndipo lilipo official gate la kuingilia hifadhi ya Serengeti kama unatokea Ngorongoro crater. Kilima unachokiona mbele yako ndio Naabi Hill na hapo ndio kuna gate na ofisi za TANAPA kwa ajili ya kutoa vibali na ukaguzi mbali mbali kwa wanaoingia na kutoka ktk Hifadhi ya Serengeti.

Licha ya kuwa gate la kuingilia hifadhi ya Serengeti lakini pia ni sehemu murua ya kupata msosi unapokuwa njiani. kipindi cha msimu wa utalii hapo panakuwa hapatoshi, inakuwa shida kupata 'kimbweta' cha kupatia msosi. wakati huo inabidi uwe na mkeka wako kama ukishindwa kupata na

Ndege wa hapa hawaogopi watu, nilishtukia kitu kikidonoa soli ya simpo zangu bila taarifa.
Jina la ndege limenitoka, mwenye data atoe msaada.

Magari ambayo madereva aidha wanakamilisha taratibu za kuingia/kutoka hifadhi au wageni wao wanapata msosi. kwa mandhari yake ilivyo, ni sehemu nzuri ya kupatia lunch.

Hata kwa wale wanaosafiri kwenda kanda ya ziwa (Mwanza au Mara) kutokea Arusha na kupitia hifadhi ya Serengeti, hupitia katika gate hili wanapoianza au kuimalizia hifadhi (kwa wanaoelekea Arusha) ya Serengeti.

1 comment:

  1. fantastic! at least blog yako iko tofauti, wengine waliobaki ni kuigana - mpaka picha wanatumia the same.

    kazi nzuri, by the way napenda mambo ya outdoor adventure.

    ReplyDelete