Tembo anategemea sana uwezo wake wa kunusa ili kuweza kutambua mazingira aliyopo na vitu vinavyomzunguka. Sambamba na harufu, tembo pia ana uwezo mkubwa wa kusikia kupitia masikio yake makubwa (by the way, tembo porini huitwa Masikio).
Tembo hana uwezo mkubwa wa kutambua vitu kwa kuona. hutegemea zaidi pua na masikio kuweza kufanikisha shughuli zake. kutokana na hali, mara nyingi ukiwa porini unashauriwa kumpiga picha tembo BILA ya kutumia flash. hii inatoka na kwamba, endapo utatumia flash wakati unampiga picha, tembo atajenga hisia ya kutoelewa nini kimetokea. kwa kifupi hataweza kutofautisha kama ni kitu cha kawaida au ni hatari. ktk mazingira haya, huanza ku-charge kuelekea upande ule ambao mwanga umetokea.
Ushauri wa bure ni kwamba hakikisha flash ya kamera yako imezimwa unapompiga picha tembo na cha msingi sana usimkaribie kwa karibu kama flash ya kamera yako ni automatic - inajiwasha yenyewe kutoka na mwanga inaoupata.

No comments:
Post a Comment