Friday, December 11, 2009

Japo nyasi ni fupi........

simba anaweza kujificha na asionekane kirahisi


Awali hatukuwaona hawa simba. siwezi kusema kama walikuwa wamejificha au la, lakini ukweli ni kwamba tuliwapita bila kuwaona. hayo ndio maajabu ya serengeti.
Ni mbuga ya Nyasi lakini hata pale ambapo kuna nyasi fupi, wanyama wanaokula wanyama wengine wana namna ya yao ya kujificha ili kuweze kufanikisha mawindo yao.

hao jamaa hapo juu wametega mingo pembeni ya hicho kibwawa kidogo chenye maji. atakae kuja kunywa maji kichwa kichwa ni halali yao.

Hali hii ndio inayopelekea kwa nyumbu na wanyama wengineo kuhama ktk mbuga hii pindi pale nyasi za eneo waliopo zikiwa ndefu na kuhatarisha usalama wao. huwa wanahamia maeneo yenye nyasi fupi ili waweze kuona mbali na kumuona adui mapema na akiwa mbali.

No comments:

Post a Comment