Oldupai ni neno la lugha ya kimasai lenye kumaanisha mmea wa Katani mwuti (wild Sisal). Mmea huu unashamiri sana maeneo ya umasaini na pia unatumika na wenyeji kama dawa.
Baada yakugundulika kwa masalia ya awali ya binadamu wa kwanza, wanasayansi walianza kwenda eneo ambalo sasa linafahamika kama Olduvai Gorge. kipindi hicho, eneo hilo halikuwa na jina kwa kuwa hakukuwa na mji au kijiji. baada ya kufanya uchunguzi wao na kugundua mabaki hayo, wanasayansi hao walihitaji kutoa jina kwa hilo eneo jina ambalo lingetumika kama refference. kwa kuwa katani mwitu ilishamiri sana eneo hilo, wanasayansi hao waliamua kuchukua jina la kimasai la katani mwitu ili walitumie ktk taarifa zao.
walipoambiwa jina la katani mwitu, aliyekuwa anaandika taarifa hizi kwa bahati mbaya akaandika Olduvai badala ya Oldupai kama Wamasai wenyewe wanavyoitamka. Bila kujua dunia ikatangaziwa kuwa sehemu hiyo inaitwa Olduvai Gorge.
hivi karibuni Serikali imeanza kuonyesha jitihada za kutaka sehemu hiyo ijulikane kama inavyotakiwa, nikimaanisha Oldupai badala ya Olduvai kama ilivyozoeleka na wengi.
unaweza soma zaidi kwenye: http://en.wikipedia.org/wiki/Olduvai
No comments:
Post a Comment