Tuesday, December 1, 2009

Ni nadra sana kukutana nae porini

Mwanzo tulimpita tukidhani ni Nyati au Nyumbu. lakini ghafla dereva aksimama na kurudi nyuma huku akituambia - hii ni habari njema, watu wanahangaika sana kumtafuta huyu myanama lakini hawampati kirahisi

Tuliposimama na ku-reverse ndio tukafahamu kuwa mnyama huyo ni Kifaru ambae alikuwa 'kajificha' katika nyasi fupi.

Awali alikimbia mbali na gari letu nakuelekea mbali kidogo na tulipokuwa, tukajua tumeshampoteza ktk upeo wetu wa macho (ukizingatia ngorongoro off road driving hairuhusiwi)

Ghafla alisimama, akageuza na kuanza kuja kasi usawa wa gari tulilokuwamo. hali hii ilimfanya dereva wetu awashe gari na kisha kuanza kusogea mbali. baada ya kusikia mmungurumo wa gari, nae alisitisha zoezi lake la ku-charge kwenye gari yetu

Black Rhino, Ngorongoro crater

Tofauti rahisi kati ya white na Black Rhino ni upana wa midomo yao. midomo ya Black Rhino (kama unaemuona hapo juu) huwa umechongoka kwa mbele. ilhali ule wa White Rhino unakuwa butu na mpana - wide.

2 comments:

  1. so refreshing, siyo kila siku kubishana siasa na porojo, ndiyo maana akili zinadumaa.

    mdau endeleza libeneke, wafuasi wako tupo.

    ReplyDelete
  2. Ni mnyama adimu sana huyu, ni vema kama serikali ikachukua juhudi za makusudi za kumtunza kwa gharama yoyote ile!

    http://jadili.blogspot.com

    ReplyDelete