Wednesday, December 30, 2009

Momella Ndogo - Arusha National Park

Kwa mbele ni moja ya maziwa yaliyopo ndani ya Arusha National Park (ANAPA). Ziwa hili inaitwa Momella Ndogo aka Small Momella. Ni ziwa ambalo maji yake ni Alkaline kama yalivyo maziwa mengine yanayopatikana ktk ukanda wa kaskazini wa utalii

Mandhari ya Small Momella ni maridhawa kwa kwenda mbele, pako tulivu. picha hii ilipigwa tokea ktk moja ya observation points pembezoni mwa ziwa hilo.

Ka-kisiwa kadogo ndani ya ziwa. Kwa kawaida, Mlima Meru huonekana vizuri sana tokea hapo picha ilipopigwa. lakini kutokana na mawingu kuwa mengi, Mlima unakuwa umefichwa kinamna.

Data kuhusu Small Momella lake. ni wachache wanaoyafahamu haya maziwa, tembea Tz inakpa dondoo ili mdau upate hamasa ya kwenda kuzuru hizi sehem sehem na kujionea mambo ya huko.

No comments:

Post a Comment