Monday, July 28, 2014

Mbudya Island Marine Reserve - Dar es Salaam

 Ni Kisiwa kinachopatikana ukanda wa pwani ya Kunduchi, Kaskazini mwa Jiji la Dar Es Salaam. Ni kisiwa ambacho kimetengwa kwa ajili ya kuhifadhi viumbe wa baharini - Marine Reserve. Licha ya kuwa ni eneo la uhifadhi, kisiwa cha Mbudya ni eneo mwanana kwa mapumziko na hata kuogelea. Kisiwa hiki kinafikika karibu kila siku kwa njia ya boti ambazo nyingi huanza safari zake kwenye hoteli zilizopo ukanda wa pwani ya Kunduchi kwa bei za kizalendo. kwakuwa hili ni eneo la uhifadhi, mgeni hulazimika pia kulipia kiingilio ufikapo kisiwani Mbudya. mbali na gharama ya usafiri wa boti.



Eneo lenye mchanga mweupe hujulikana kama Beach One. Upande wa pili wa Kisiwa kuna pwani nyingine ya mapumziko ijulikanayo kama Beach two. Boti nyingi zinazofanya safari za kupeleka wageni Kisiwa cha Mbudya huweka nanga na kushusha abiria wake upande wa beach one. kufika Beach two, ambako huwa kunakuwa na watu wachache ni kwa kutembea kwa miguu. Unakatisha huo msitu wa miti katikati ya kisiwa na kuibukia beach two. Binafsi sijawahi fika beach two japo rafiki zangu kadhaa wamefika huko na kunieleza ya kuwa safari ya kwenda beach two ni adventure ya namna yake pia.


Ukidodosa vyema unaweza kuona vibanda vya Misonge ambako wageni hupata fursa ya kupumzikia.

No comments:

Post a Comment