Monday, July 28, 2014

Utafungua au utaacha???

Unapokuwa unaangalia wanyama ndani ya Dar Es Salam zoo, pembezoni ya vibanda walivyohifadhiwa nyoka wa aina mbalimbali unakutana na hili tangazo na mlango unaoonekana kwenye picha. Maelezo ya tangazo yanakuelekeza kufungua mlango ili uweze kumuona mnyama hatari zaidi hapa duniani. Wewe utathubutu kufungua au utakubali yainshe kinamna bila ya wewe kumjua huyo mnyama?

No comments:

Post a Comment