Friday, April 18, 2014

Mto Rufiji jioni ya leo (18-Apr-2014)

Rufiji River, Tanzania - Kanuth Adventures
Ni Picha zilizopigwa jioni hii ya Leo na kutufikia muda mfupi iliopita zikionyesha Mandhari mwanana ya Mto Rufiji. Picha hizi zimepigwa pembezoni ya mto Rufiji, Hippo Campsite iliyopo kwenye kijiji cha Mloka nje kidogo ya pori la akiba la Selous. Mdau Kanuth yupo huko na ndio chanzo cha picha hizi. Hali ya mto inaridhisha sasa hivi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo kadhaa hapa nchini. Awali hali ilikuwa mbaya kwani kina cha maji kilikuwa kimepungua sana mpaka boat safaris zilikuwa zikifanywa kwa taabu na kipindi kingine kushindikana kabisa. Wanyama waliokuwa wanutegemea mto ili kuishi nao walikuwa wanataabika huku wengine wakihama maeneo yao ya kujidai. Hali ilikuwa mbaya kwa wananchi wanaoishi pembezeni ambao huutegemea mto Rufiji kama chanzo cha maji na njia ya usafiri. Unaweza ku bofya hapa kujionea vyema picha za hali ilivyo kuwa mwezi Novemba mwaka jana.Rufiji River, Tanzania - Kanuth Adventures

Rufiji River, Tanzania - Kanuth Adventures

Rufiji River, Tanzania - Kanuth Adventures
Picha zote kwa Hisani ya Mdau Kanuth Tarimo wa Kanuth Adventures

1 comment: