Saturday, November 23, 2013

Kina cha maji kimepungua Mto Rufiji


Rufiji River Tanzania
 Ni Picha za wiki hii nilizotumia na mdau Kanuth zikionyesha baadhi ya maeneo ya Mto Rufiji kwenye kijiji cha Mloka huko Rufiji. Sina haja ya kusema maneno mengi lakini kwa hali inayoonekana ni dhahiri hali ya kina cha maji kwenye mto huu imefikia kina cha chini mno. Huu ni mto ambao wageni huwa wanatembezwa kwa maboti kwenye zile boat safaris. Sasa hivi hata hizo boat safaris zinafanywa kwa nadra na kwenye eneo dogo. Wageni wanalazimika kutembea kuifuata boat mahali ambapo kina cha maji kinaiwezesha kuanza safari. Sehemu ambazo majani yameota ni sehemu ambazo kwa kawaida huwa zimefunikwa na Maji kipindi ambacho si cha kiangazi. Kukupa picha ilivyo, naomba urudie posts hizi kadhaa za mto huu ambazo zinaonyesha hali inavyokuwa kipindi kingine cha mwaka.


Rufiji River Tanzania
Kwa kawaida hapa maji huwa yanakuwa yamejaa mwanzo mwisho. sasa hivi ni visiwa vya mchanga na majani

Rufiji River Tanzania

Rufiji River Tanzania

Rufiji River Tanzania

Rufiji River Tanzania

Rufiji River Tanzania
Hapo inatafutwa sehemu ya kuegeshea boat ili wageni waweze kupanda na kuanza boat safari. kwa kipindi cha kawaida eneo hili huwezi kulifikia kwa kutembea kwa miguu.
Shukran ya picha kwa Mdau Kanuth wa Kanuth Adventures

No comments:

Post a Comment