Tuesday, April 29, 2014

Moja ya tofauti kati ya Mbega wekundu wa Zanzibar na Ngedere

 Visiwa vya Zanzibar vinaelezwa ya kuwa ni Visiwa pekee ambako Mbega wekundu wanapatikana duniani mpaka kufikia hatua ya mbega hao kupewa jina la Zanzibar red colobus monkey. Inaelezwa ya kwamba Mbega wekundu wapo kwenye orodha ya wanyama walio hatarini kutoweka kwenye sura ya duniani kutokana na idadi yao kupungua kwa kasi. Kwenye kisiwa cha Unguja, msitu wa Jozani ni moja ya maeneo ambako unaweza kuwaona. Ni msitu maalum kwa ajili ya kuwahifadhi mbega hawa na viumbe hai wengine. Nilimuuliza Guide tuliyetembea nae ndani ya msitu wa Jozani moja ya tofauti kati ya Mbega na Ngedere (tuliowazoea huku bara). Alinieleza kuwa Mbega wana vidole vinne kwenye mikono yao wakati Ngedere wao wanakuwa na vitano kama binadamu. Picha hizi mbili ni baadhi ya picha chache nilizoweza kuzipiga kuonyesha hali halisi ya idadi ya vidole ya Mbega wa Zanzibar. Utaona ni dhahiri Mbega hawa hawana kidole gumba kwenye mikono yao.



Huyu ni mwingine akionekana kwa angle nyingine. Miguu yao ina vidole vitano kama walivyo ngedere.

1 comment:

  1. Asante mungu kwa kutupatia utajiri wa kila namna hii ndio Tanzania wageni wanayoitamani

    ReplyDelete