Tuesday, October 8, 2013

TANAPA Bandas - Saadani National Park


TANAPA Bandas Saadani National Park Bagamoyo Tanzania
 Kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani, TANAPA wanamiliki na kusimamia Rest house, Bandas na Campsite. awali niliwahi kurusha picha ta TANAPA Rest House (Bofya hapa kama ulizikosa). Hii post ina picha ya Bandaz za TANAPA za Saadani NP. Bandaz zinakuwa na vyumba viwili, self contained. Kila chumba kina vitanda viwili. Picha juu ni moja ya bandas ambalo lina vyumba viwili tofauti, kila kimoja kikijitegemea kwa mahitaji yake. Bandas zina umeme wa SolarTANAPA Bandas Saadani National Park Bagamoyo Tanzania
Bandaz zipo tano na kila mmoja ina vyumba viwili vya kulala wageni. Jengo linaloonekana kulia ni mess ya kulia chakula pamoja na jiko la kuandalia maakuli.

TANAPA Bandas Saadani National Park Bagamoyo Tanzania
Mess ya kulia chakula ikonekana kwa ukaribu

TANAPA Bandas Saadani National Park Bagamoyo Tanzania
Ni Pwani ya bahari ya Hindi ambayo haipo mbali na hizi bandaz, ni mwendo wa kutembea kwa mguu na unakuwa umeingia kwenye mandhari ya pwani ukitokea kwenye mandhari ya Porini.

TANAPA Bandas Saadani National Park Bagamoyo Tanzania
Pwani mwanana ya Saadani huko Bagamoyo. Hii hapa ni bado ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani. Saadani ni hifadhi pekee Africa ambayo inapakana na Bahari.

TANAPA Bandas Saadani National Park Bagamoyo Tanzania
Jengo la mess likionekana kwa kati sambamba na baadhi ya Bandaz zikionekana kwa nyuma yake.

TANAPA Bandas Saadani National Park Bagamoyo Tanzania
Kulia ni Bandaz na Kushoto ni Rest House. Hivi viwili vipo karibu na kinachotengenisha ni hiki kichaka unachokiona katikati. Endapo wageni hamtatosha kwenye Rest house baadhi wanaweza wakalala Bandas.
infosaadani@tanzaniaparks.com Ndio email ya wahifadhi wa Saadani endapo utapenda kujua na kupanga safari yako kwenda Saadani

No comments:

Post a Comment