Monday, September 9, 2013

TANAPA Rest house, Saadani National Park - Bagamoyo

 TANAPA Rest house Saadani National Park Tanzania
Ni Rest house ambayo imejengwa na kuendeshwa na TANAPA ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadani. tofauti na hotel nyingi za kitalii, hii imejengwa kwa mtindo wa nyumba za kawaida tulizozizoea wengi. Ina vyumba 3 vya wageni, vyote vikiwa ni Self contained. Jiko, mesi ya kulia chakula na choo cha Uma. Umeme upo muda wote ambapo ni wa Solar. TV ni mwendo wa Dijitali, DSTV ndani ya nyumba. Picha juu ni sehemu ya Sebule. Mgeni unaweza kuja na vyakula vyako mwenyewe na wenyeji wakakupikia na kukiaanda vile utakavyo. Mpango mwingine unaweza kupanga na wahusika ambao ni ofisi ya utalii ya Hifadhi ya Saadani.

 TANAPA Rest house Saadani National Park Tanzania
Huu ni muonekano wa Rest house kwa mtu anayetokea beach. Vyumba vya wageni (vitatu upande wa Kulia) vina milango ambayo mgeni akitaka kwenda pwani anatokea chumbani na kuchapa mwendo kuelekea baharini.

 TANAPA Rest house Saadani National Park Tanzania
Booking za kufikia kwenye hii Rest house, Bandaz au Campsite vyote vikiwa vya TANAPA vinafanywa kupitia ofisi ya Utalii ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani; infosaadani@tanzaniaparks.com 

1 comment:

  1. This blog is very helpful.....had a last minute booking for Saadani and didn't know where to take my budgeted clients....and there came Tembe Tz....
    loved it.............:)

    ReplyDelete