Tuesday, October 1, 2013

Serengeti Migration; Imeanza kurejea Tanzania

Ni Picha zilizopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita pembezoni ya Mto Mara, zikionyesha Nyumbu wa Serengeti wanaohama wakirejea ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti, Tanzania wakitokea Hifadhi ya Maasai Mara nchini Kenya. Wanarudi kuwahi nyasi za awali baada ya mvua ambazo nimeelezwa ya kuwa zimeshaanza kunyesha ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo jiraniWakijipanga na kushauriana kabla ya kuvuka Mto Mara na kuingia rasmi ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti

Wale wenye uthubutu wakitangulia huku wenzao wakijipanga kuwafuata ili waweze kuingia majini na kuuvuka mto. Ieleweke ya kwamba, kikubwa kinachowaleta hawa Nyumbu kwenye hifadhi ya Serengeti ni uwepo wa majani (chipukizi) ambayo ndio chakula kinachopendwa na wanyama. Majani haya huanza kupatakana mara baada ya mvua kuanza kunyesha.

Safari inaendelea

Safari yao ni ya mafungu kama vile anavyopenda kusema Mwenyekiti wa Jukwaa la MjengwaBlog; Nyumbu wa Serengeti nao pia huwa wanasafiri kwa mafungu pia. hapa linaonekana kundi moja kufika upande wa pili wa Mto huku kundi jingine likijipanga kuanza kukabiliana na Mto ili kuuvuka.Hawa wameshavuka na kuingia kwenye ardhi ya Tanzania


Shukran ya picha kwa mdau Bonny wa Arusha

No comments:

Post a Comment