Thursday, October 3, 2013

Ngorongoro crater view Point

Ni sehemu ambayo wengi wanaoenda Ngorongoro crater hupata fursa ya kuiona crater vizuri kwa mara ya kwanza. Hususan wale wanaotokea Arusha na Karatu. Ni sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya kuweza kujionea maajabu ya eneo hili kwa juu kabla ya kuteremka na kuingia ndani ya crater na kushuhudia maajabu yenyewe kwa karibu zaidi.Ziwa Magadi likionekana kwa mbali ndani ya Crater. Kwa lugha ya wazee wa porini, Ngorongoro crater hujulikana kama shimoni. Ni moja ya maeneo ya uhifadhi hapa Tanzania ambako mgeni anakuwa na nafasi kubwa ya kuona kifaru.

Shukran ya picha kwa Mdau Thomas wa HSK Safaris, DSM

No comments:

Post a Comment