Monday, September 30, 2013

Mfalme wa Porini - Serengeti

Ni picha ya Sharubu (Simba) iliyopigwa ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Kutumwa kwetu na Mdau Bonny. Ni Sharubu dume aliyekuwa amepumzika chini ya mti akiweka sawa mipango yake ya mawindo. Mnapokuwa mnaingia kwenye hifadhi, wengi huwa na shauku kubwa kumuona mzee wa pori. lakini sightings kama hizi zinapotokea, usishangae nusu ya abiria gari mliomo wakianza kuomba muondoke eneo hilo. Hawa jamaa waone kwenye TV tu, wanamvuto lakini pia wanatisha. Usiombee aungurume wakati mpo karibu yake.

 


No comments:

Post a Comment