Tuesday, October 29, 2013

Flamingo wa Ziwa Momella, Arusha National Park


 Flamingo huwa na tabia ya kuhama kufuatana na mazingira wanayohitaji. Moja ya vituo vyao ni kwenye hifadhi ya Arusha hususan kwenye maziwa ya Momella. Kwakuwa maji ya Ziwa hili ni Alkaline, maji haya yanawavutia algae ambao ni chakula kikuu cha Flamingo.






Ziwa la Momella (Kubwa) lipo kwenye mpaka wa Hifadhi ya Taifa na Kijiji cha Maji ya Chai. Uzio unaouona ndio alama ya mpaka na vibanda vinavyoonekana kwa pembeni ni nyumba za wanakijiji ambazo zipo nje ya hifadhi.


No comments:

Post a Comment