Thursday, October 31, 2013

Lunch time ndani ya Selous Game Reserve

mara nyingi wageni hubeba chakula watakachokula pindi wanapoondoka hotelini asubuhi. Dhumuni kuu la mpango huu ni kupunguza safari ya kutoka kule wanapokuwa na kurudi mpaka hotelini au campsite na baadae kuendelea tena. Mnapokuwa mnaondoka asubuhi, wahudumu wa hoteli hufanya mawasiliano na dereva wenu na kuwaandalia chakula cha kubeba, Lunch box. Baadhi ya hoteli huwa na menu maalum ambazo wageni mnapewa kuchagua kile mnachokipenda kuandaliwa kwenye lunch box zenu. Kila pori lina sehemu zake maalum zilizotengwa kwa ajili ya kulia maakuli ya mchana - picnic sites. Hapo wageni wanaweza kushuka kwenye gari, kujinyoosha na kukaa njea ya gari. Japo maeneo mengine wageni wanaweza egesha gari na kula chakula chao lakini hawatakuwa na ruhusa ya kushuka kwenye gari na endapo watafanya hivyo basi wanaweza tozwa fine kwa kushuka nje ya gari ukiwa ndani ya eneo la hifadhi. Kwenye hifadhi za Taifa, picnic sites huwa na maliwato kwa wale wataohitaji huduma hiyo.


 Kulingana na hali ya usalama ilivyo na uchovu mlionao, wageni hupata fursa ya kula chakula na wakati mwingine hata kula siesta (kama muda unaruhusu) kamba ambvyo wageni hawa wanavyoonekana. Hapo walikuwa pembezoni ya ziwa Manze huko Selous Game Reserve, Rufiji.

Picha kwa hisani ya Mdau Thomas wa HSK Safaris

No comments:

Post a Comment