Ni Picha kadhaa zenye lengo la kukuonyesha baadhi ya mambo ambayo unaweza kuyaona na kujifunza ukifanya boat safari kwenye mto Rufiji huko Mloka, nje kidogo ya pori la akiba la Selous. Kwa Selous, boat safaris zinaweza kufanywa nje ya eneo la hifadhi au ndani ya pori. Ndani ya pori la akiba, ni campsite kadhaa ndio zenye vibali vya kufanya shughuli hii kwenye baadhi ya maziwa yaliyomo huko. kwa huku nje karibu campsite zote zinatoa huduma hii kwa wateja wao. Kwa wengi, Boat Safari hufanywa muda wa asubuhi au jioni baada ya game drive au mapumziko. Muda wa jioni huwa ni mzuri zaidi kwani ni muda ambao wanyama kama kiboko huwa ndio wanaanza kuchomoza wakijiandaa kutoka nje ya mto kwenda kutafuta chakula.
Kwa wanaopenda kuangalia ndege, huwa wanapata fursa ya kuona baadhi ya ndege kwa ukaribu mkubwa zaidi. Ndege huwa wanakuwa wamejenga viota vya kwenye hivi visiwa vyenye matete ndani ya mto. Wakati wa safari guide au captain wa boti anakuwa anatoa maelezo ya wanyama, ndege na mambo mbalimbali yanayouhusu mto Rufiji na wanyama wa porini pia.
Weaver bird au ndege mnana kwa kiswahili
Huyu hapa akiwa anawajibika kwenye ujenzi wa kiota chake
Kingfisher akiwa anawalia timing samaki
Kwakuwa hii safari ya boat ilifanyikia kijijini, unapata fursa pia ya kukutana na wanakijiji wakiwa kwenye usafiri na shughuli zao za kila siku. huu ni usafiri unaotumika kuwavusha kutoka upande mmoja wa mto rufiji kwenda mwingine. Hapa ni kundi la akina mama likiwa na captain wa mtumbwi wao wakiendelea na safari yao ndani ya mto Rufiji
Shukran ya picha - Mdau Thomas wa HSK Safaris
No comments:
Post a Comment