Wednesday, August 21, 2013

Oldonyo Lengai

Oldonyo Lengai Tanzania
Ni moja ya milima iliyopo Afrika ya Mashariki ambayo volcano yake bado ipo hai (Active volcano). Hii inamaanisha Volcano ya kwenye mlima huu inaweza kulipuka muda wowote kama ilivyotokea miaka kadhaa iliyopita hali iliyopelekea wakazi wa maeneo jirani kuhamishwa. Kwa jamii ya Wamasai, mlima huu unajulikana kama Mlima wa Mungu, na ndio maana ya Jina lake. Mlima huu upo ndani ya eneo linalosimamiwa na Mamlaka ya Ngorongoro conservation Area Authority (NCAA). Kumbuka ya kwamba eneo liliopo chini ya NCAA lina upekee wa namna yake ambapo Wanyama wa porini na Binadamu wanaishi pamoja. Picha juu ni mlima huu unavyoonekana tokea angani (kwenye ndege)

Oldonyo Lengai Tanzania
Wapo ambao wanaupanda huu mlima na Safari yake huchukua siku moja. hamna kambi za kulala na upandaji wake ni tofauti na ule wa Mlima Kilimanjaro. Safari huanza Alfajiri na mgeni anarudi jioni/usiku. Sio mlima mrefu sana lakini hali yake ya mwinuko ni kikwazo kwa wengi na kufanya zoezi la kuupanda kuwa gumu. Ukienda Google jaribu kusearch kwa kutumia keyword ya "Oldonyo Lengai climb" na utapata list za makampuni kedekede ya Utalii yanayopandisha wageni kwenye huu mlima

Oldonyo Lengai Tanzania

1 comment:

  1. It's a beautiful picture. I think it's not easy to get a picture of this mountain in the clear day.
    I enjoy sight seeing in this site. Thank you for sharing this awesome pictures. Although i don't understand the languange.
    Thank you again.

    ReplyDelete