Tuesday, September 3, 2013

Geti la Wami - Hifadhi ya Taifa ya Saadani

Wami Gate - Saadani National park
Ni Kituo kijulikanacho kama Geti la Wami, eneo ambalo mgeni anaingilia ndani ya hifadhi ya taifa ya Saadni kwa upande wa wilaya ya Bagamoyo. Hili Geti litatumika kwa yule aliyeingilia kwa kupitia njia ya Bagamoyo - Msata. Aliyekaa ni Mfanyakazi wa hifadhi akituandikia kibali cha kuingilia kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadani. Geti hili lipo pembezoni ya mto Wami.

Wami Gate - Saadani National park
Hifadhi ya Saadani ipo kilometa 120 tokea Dar (kwa njia ya Bagamoyo-Msata).

Wami Gate - Saadani National park
Japo ndio tulikuwa tunakamilisha utaratibu wa kuingia ndani ya hifadhi, Hawa nguchiro waliokuwa wengi walitukaribisha kwa mbwembwe na pilika pilika zao lukuki pembezoni ya ofisi za wasimamizi wa hifadhi.

No comments:

Post a Comment