Wednesday, August 21, 2013

Ni Mto Mara....

Mto Mara
Siku kadhaa zilizopita niliwauliza wadau mjaribu kubashiri jina la mto unaonekana kwenye picha hii. Hakuna aliyejaribu, pengine swali limekuwa gumu sana. Kwa kuwa lengo ni kuelimishana ili kuweza kuifahamu nchi yetu vyema basi sina budi kuweka bayana jina la mto huu. Ni mto Mara na hapo ni mahali ambapo mto huu unaingia Ziwa Victoria. Unachikiona kwa mbali ni Ziwa Victoria. Mto huu unaanzia nchi jirani kwa watani zetu wa jadi (+254) na baadae unaingia nchini kwenye hifadhi ya Taifa la Serengeti eneo ambalo huvutia wageni wengi kuangalia jinsi wanyama wanaohama wanavyohaha kuuvuka.

Mto Mara
Sehemu iliyozungushiwa duara jekundu ni sehemu ambayo mto Mara unakuwa unachora kitu chenye muonekano kama Moyo aka Kopa. Shukran kwa Mdau Albert aliyepiga picha hizi hivi karibuni akiwa safarini Mkoa wa Mara.
Unaweza kusoma zaidi habari za mto huu kwa kubofya hapa

No comments:

Post a Comment