Sunday, April 28, 2013

Mapito ya wapanda mlima Kilimanjaro kwa njia ya Marangu kati ya Mandara na Horombo

Marangu route Mandara to Horombo
Ni picha zenye kuonyesha mapito wanakopita wapanda mlima Kilimanjaro (Marangu route) kuanzia kituo cha Mandara kuelekea kituo Horombo. Kwa maeneo haya hali ya uoto ni Nyasi na baadhi ya maeneo kunakuwa na miti pembezoni, lakini unavyozidi kupanda kuelekea juu uoto wa eneo hubadilika na kuna sehemu hakuna nyasi wala majani kabisa. Kwa maeneo haya, Njia za kupita zinakuwa zimechongwa na kuonekana kama zinavyoonekana katika picha kadhaa kwenye hii post. Maeneo ya Saddle kuelekea kibo na huko mbele hali ni tofauti na ilivyo maeneo haya.

Marangu route Mandara to Horombo
 Ni Msitu mdogo uliopo mita kadhaa baada ya kupita njia panda ya kwenda Maundi Crater.

Marangu route Mandara to Horombo
 Vigingi vipo, na inabidi uvikwee kwa upole...

Marangu route Mandara to Horombo
 Somo la uoto wa asili linakuwa linajidhihirisha waziwazi ukiwa unapanda Mlima Kilimanjaro. Unavyozidi kupanda, unabaini jinsi miti na majani yanvyopungua na miti unayokutana nayo huku juu ni tofauti na ile uliyoiona ukiwa maeneo ya chini. Nakumbuka shule ya msingi na hata sekondari kwenye somo la Jiografia tulikuwa tunatumia nguvu nyingi sana kuweza kusoma na kuelewa (wakati mwingine tulikariri) mambo yanayohusu uoto wa asili (Natural Vegetation) wa maeneo ya pwani, kanda ya kati na maeneo ya nyanda za juu.

Marangu route Mandara to Horombo
Safari inaendelea...

Marangu route Mandara to Horombo
Siku hii hali ya hewa ilikuwa inabadilika mara kwa mara. Mawingu na manyunyu ya hapa na pale yalikuwa yakija kila baada ya masaa kadhaa

No comments:

Post a Comment