Sunday, April 28, 2013

Kutoka Mandara hut kuelekea Horombo hut - Marangu Route

Mandara to Horombo - Marangu route
 Eneo linalozunguka kituo cha Mandara kuna uoto wa misitu. Picha juu ni Mdau Frank (Kulia) akiwa na Ahsantiel, Mmoja wa guide tuliyekuwa nae wakiwa kwenye ki msitu muda mfupi baada ya kutoka Kituo cha Mandara kuelekea Horombo. Ukianza safari yako mida ya mapema unapofika maeneo haya unaweza kubahatika kukutana na Mbega weupe.

Mandara to Horombo - Marangu route

Mandara to Horombo - Marangu route

Mandara to Horombo - Marangu route

Mandara to Horombo - Marangu route
 Njia panda ya kuelekea Maundi Crater, Ni kivutio kilichopo mita kadhaa kutoka kituo cha Mandara ukiwa unaelekea Horombo. Unapofika Maundi crater unaweza kuona maeneo kadhaa yaliyopo pembezeni ya mlima Kilimanjaro ikiwemo maeneo yaliyopo kwa watani wetu wa jadi. Siku ya kupanda hali ya hewa ilikuwa ya mawingu sana kwa hiyo hatukupita Maundi crater badala yake tulinyoosha kuelekea Horombo tukiwa na mkakati wa kupita Maundi Crater wakati wa kushuka 

Mandara to Horombo - Marangu route
Vituo vya hapa na pale vilikuwa vingi ili kuweza kujua mawili matatu kuhusu mlima Kilimanjaro na mazingira yake.

Mandara to Horombo - Marangu route

Mandara to Horombo - Marangu route

Mandara to Horombo - Marangu route
 Safari ya kuelekea kituo cha Horombo ikiendelea.....

No comments:

Post a Comment