Monday, March 25, 2013

Mandhari ya Kituo cha Kibo Hut

Kibo Hut, Mount Kilimanjaro Tanzania
Ni picha za majuzi tu (22 March 2013) wakati tukiwa tunaondoka kibo Hut kurudi Horombo Hut. Hii ilikuwa ni mida ya asubuhi na unachokiona kama unga mweupe chini ni theluji iliyodondoka usiku kucha wa siku hii.

Kibo Hut, Mount Kilimanjaro Tanzania
 Kilele cha Kibo kikionekana kwa nyuma, Juu ya kilele cha Kibo ndio kuna kituo cha Gilmans na kile maarufu kabisa cha Uhuru.

Kibo Hut, Mount Kilimanjaro Tanzania
Hili ndio banda la kulalia wageni wanaopanda na kushuka kwa kupitia njia ya Marangu. Ndani ni kama bweni ambako kila chumba kina vitanda vya ghorofa na kila chumba kinachukua wageni kuanzia 14 mpaka 20. Wapandaji wa njia ya Rongai wao hawalali ndani ya hili jengo bali wao na timu zao wanalala kwenye mahema wanayokuwa nayo na kumaliza mambo yao yote kwenye mahema yao.

Kibo Hut, Mount Kilimanjaro Tanzania
Kilele cha Mawenzi kikionekana kwa mbali tokea kituo cha Kibo. Siku hii theluji ilianguka ya kutosha kiasi cha kukipa kilele cha Mawenzi shuka jeupe la theluji jambo ambalo si kawaida sana kwa kilele cha Mawenzi.

Kibo Hut, Mount Kilimanjaro Tanzania
Haya ni mahema wanayotumia wapanda mlima wanaotokea njia ya Rongai. Kituo cha Kibo kinakutanisha njia mbili za kupandania mlima Kilimanjaro, Marangu na Rongai. Lakini kwa kuwa wale wa njia ya Rongai wao wanatumia mahema, wafikapo Kibo wao huendelea kulala kwenye mahema sambamba na timu zao za waongozaji na wabeba mizigo yao kama inavyoonekana kwenye picha hii juu. Hema kubwa ni hema walilokuwa wamelala wasindikizaji huku mgeni wao akiwa kwenye hema dogo la njano.

Kibo Hut, Mount Kilimanjaro Tanzania
Mimi (kushoto) nikiwa sambamba na Mdau Frank (kulia) tukijiandaa kuanza safari ya kurudi Kituo cha Horombo kutokea Kibo. 


3 comments:

  1. kwa kweli TANZANIA NI NZURI TUNAKOSA WATU MAKINI TU WA KUTUTOA KWENYE LINDI HILI LA UMASIKINI

    ReplyDelete
  2. mungu ibariki kilimanjaro mungu ibariki tanzania

    ReplyDelete
  3. mungu ibariki kilimanjaro mungu ibariki tanzania

    ReplyDelete