Monday, March 25, 2013

Kilele cha Kibo

 Ni taswira nilizozipiga siku ya Ijumaa asubuhi nikiwa njiani kurudi kituo cha Horombo kutoekea kituo cha Kibo. Ilikuwa ni safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa njia ya Marangu, Safari ambayo ilianza siku ya tarehe 18 March na kufikia tamati siku ya 23 March 2013. Picha zimepigwa kilometa chache tokea kilipo kituo cha Kibo hut, kituo ambacho ni cha mwisho kwa mpandaji wa njia ya Marangu na Rongai, kabla hajaanza kupanda kilele cha barafu siku ya mwisho kuelekea vituo vya Gilmans na mwishowe Uhuru.

Safari hii haukuwa bahati yetu kuweza kufika kileleni kabisa kwani tulilazimika kusitisha zoezi la kuelekea kileleni tulipofika mita 5100 juu ya usawa wa bahari kutokana na hali za kimwili na kiafya kuanza kwenda mrama kutokana na mwili kushindwa kuhimili vishindo vya urefu tuliofikia wakati wa safari. Tulifika Kibo Hut salama, lakini usiku tulipoanza safari ya kuelekea kileleni ndio tulikutana na hayo mauzauza ya Mlimani

Licha ya kutofika kileleni, bado tuliweza kuona na kujifunza mengi sana kuhusu mlima huu adhimu sio tu kwa hapa Afrika bali duniani kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment