Tuesday, February 5, 2013

Bukoba; May 2007

Leo nilikuwa naperuz kwenya folders za zamani na kujikuta naangukia kwenye picha yangu ya Mwaka 2007 niliyopigwa pembezoni ya Ziwa Victoria, Mkoani Kagera kwenye Mji wa Bukoba. Hapa ni karibu kabisa na Bukoba Club. Kisiwa kinachoonekana kwa nyuma ni kisiwa cha Musila. Hii safari ilikuwa na changamoto nyingi, mojawapo ilikuwa ni Camera iliyobebwa kupata hitilafu na kushindwa kufanya kazi. Hitilafu iliyogundulika tukiwa njiani kuelekea (Arusha) Bukoba Kupitia Nairobi na Kampala. Picha zote tulizopiga tulizipiga kwa kutumia Simu ya mkononi. Hii  ni moja ya picha nilizoweza kuzibaini kwenye archives zangu. Ukiachia hayo, hii Safari ilikuwa ni kama mzunguko ambapo tulienda kwa kutumiausafiri wa Bus kwa kupitia njia ya Moshi-Arusha-Nairobi-Kisumu-Naivasha-Busiya-Kampala-Mtukula mpaka Bukoba. Na kisha kurudi Dar kwa Kupitia njia ya kati; Kahama, Tinde, Igunga, Singida Mjini, Manyoni, Dodoma, Moro mpaka Dar.

No comments:

Post a Comment