Tuesday, February 5, 2013

Mandhari ya Campsite namba 1, Mikumi National Park

Mikumi National Park, Campsite 1
Mtundiko huu unakuletea mandhari na muonekano wa Campsite no 1 iliyopo Mikumi National park. Picha juu ni moja ya maeneo mawili ambayo wageni wanaweza kuweka kambi na kulala wakiwa ndani ya hifadhi. Eneo la kwanza ni hilo linaloonekana lilipoegeshwa hilo Lori la Lakeland Africa. Eneo la pili lipo upande wa kulia baada ya kupita kibanda kilichoezekwa kwa bati kinachoonekana kwa mbali kulia. Hicho kibanda ni kibanda kwa ajili ya huduma binafis (maliwato). Kwa nyuma ya Lori ni kibanda kingine kidogo ambacho hutumika kama jiko na kinatumiwa na wakazi wa maeneo yote mawili. Wageni wanakuwa huru kuchagua namna na jinsi wanavyotaka kuyajenga mahema yao kwenye campsite. Ni uhuru ambao mgeni anakuwa nao endapo atafanya mobile tented camping.

Mikumi National Park, Campsite 1
Hili ni Jiko kwa ajili ya kuandalia maakuli. Kibanda ni muhimu ili kutoa usalama wa vyakula dhidi ya wanyama wasumbufu kama nyani na ngedere. Jiko ni shared baina ya maeneo mawili ya camping ktk campsite namba 1.

Mikumi National Park, Campsite 1
Picha hii nimeipiga nikiwa nimesimama mbele ya Jiko

Mikumi National Park, Campsite 1
Chumba kwa ajili ya huduma binafsi. Moja ya vitu ninavyoweza kuwapongeza wahifadhi wa mikumi ni kuhusu tulioukuta kwenye hiki kibanda. Kilikuwa kisafi kikiwa na huduma zote tofauti na mategemeo yetu kwani tulidokezwa kuwa zamani ilibidi wanaoleta wageni watembee na vifaa vya usafi ili wageni wao wasikwazike. Kwa  mikumi tulikikuta kikiwa kisafi na maji yalikuwepo muda wote.

Mikumi National Park, Campsite 1
 Picha hii inatoa taswira nzuri ya campsite namba 1 kwani unaona eneo la kwanza la kuweka camp (Chini ya mti lilipoegeshwa lory la Lakeland Africa) na eneo la pili ambalo lipo upande wa kulia wa kibanda cha maliwato. Upande huo nao una miti yake ya kivuli japo sio mkubwa kama huu uliopo kwenye eneo lilipoegeshwa lory. Kama ukibanwa unalazimika kwenda kwenye kile kibanda ili uweze kufanya shughuli zako binafsi. iwe mchana au usiku wa giza nene...

Mikumi National Park, Campsite 1
Hili ni eneo jingine la kuwekea camp ambalo nalo ni sehemu ya campsite namba 1. Wadau waligoma kabisa kuweka kambi upande huu kwa kuwa imezungukwa na miti kila upande na kuhofia kunyemelewa bila taarifa.

Mikumi National Park, Campsite 1
Maongezi na mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea baada ya kumaliza kupata staftahi huku tukisubiri muda usonge tuanze safari ya kurudi Dar.

Mikumi National Park, Campsite 1
Mahali ambapo Lori lilipoegeshwa ni kama ndio geti la kuingilia gari kwenye campsite.

Mikumi National Park, Campsite 1
Kibanda cha Vocha.. kwenye shughuli nyingine za kijamii hujulikana kama Majiografia. Hiki kina pande mbili ambako kila upande kuna bafu na choo. hii inatokana na ukweli ya kwamba campsite hii imejengwa kuwa kuhudumia makundi mawili tofauti ya campers. Kuna ambao wanaweza wakatumia upande wa kushoto, chini ya mti ambako safari hii tulikutumia sisi. au upande wa Kulia ambako napo kuna eneo jingine la kuweka kambi.

No comments:

Post a Comment