Tuesday, December 18, 2012

Walking Safari around Campsite inside Selous Game Reserve

Ni Kundi la wageni waliofanya camping ndani ya pori la akiba la Selous hapa wakifanya safari ya miguu ndani ya pori la akiba pembezoni ya moja ya maziwa yaliyopo ndani ya pori hili. Unapopewa kibali cha kufanya camping katika campsite ndani ya hifadhi, wahifadhi huwajibika kukupatia ulinzi. Kutegemea na idadi ya wageni, wahifadhi hutuoa ranger mmoja au zaidi ambaye huambata na wageni kipindi chote cha safari yao ya camping. Ranger huwa na silaha kwa ajili ya usalama. Uwepo wake na kibali kinawapa fursa pia wageni kuweza kuyaacha magari yao na kisha kutembelea hifadhi kwa miguu huku wakisindikizwa na ranger. umbali wa matembezi hutegemea uwezo wa wageni kumudu safari za miguu na pia Ranger na guide kuangalia hali ya usalama kama kuna uwepo wa wanyama hatarishi wasiotabirika. Tembo, mmoja au kundi ni mmoja ya wanyama hatari sana kukutana nae ana kwa ana kwenye walking safari. Nyati aliyepeke yake nae ni hatari pia.

Hapa wakirejea kambini baada ya matembezi. Ni namna moja ya kutembelea hifadhi ambayo inamweka mgeni moja kwa moja kwenye mazingira ya wanyama wa porini.

Akina mama ma-ranger nao wapo. Safari hii wageni hawa walikuwa na Ranger mwanamama.

Picha zote toka kwa Mdau Rajab wa Wildness Safaris Tanzania.

No comments:

Post a Comment