Monday, December 31, 2012

Pango la Misakazi

Kutokana na reli ya TAZARA kupita maeneo yenye milima, baadhi ya maeneo wakandarasi waliamua kutoboa milima ili reli na treni yake vipite ndani ya mapango kama hili la Misakazi. Hili ni pango la kwanza kukutana nalo kama mnatokea dar kuelekea Mbeya na Zambia. Japo waliyoizoea reli hii wanasema maeneo ya Morogoro na mbele zaidi yapo mapango makubwa zaidi na ambayo treni hukaa ndani kwa muda mrefu. Kwa hili la Misakazi treni hukaa takriban dakika 1.

Kama taa za kwenye mabehewa zinakuwa hazijawashwa basi hali huwa ni giza totoro. Safari hii waandaji walihakikisha taa zimewashwa ili kutoa mwanga kipindi treni ikiwa ndani ya pango hili. Kwa safari ya kwenda Selous/kisaki, hili ni pango pekee ambalo treni inapitia. Mengine yapo mbele zaidi.


Hapa treni ikitoka nje ya pango la Misakazi. Lipo mkoa wa Pwani wiliya ya Kisarawe

No comments:

Post a Comment