Sunday, December 16, 2012

Overland bugdet trip with Lakeland Africa Limited

 Ni Safari ya siku 14 ambayo itawapeleka watanzania wenzetu kwenye vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini. Safari hii ilianza rasmi jana kwa kuelekea Hifadhi ya taifa ya Saadani. Sehemu nyingine ambazo wadau watatembelea ni Pangani, Lushoto, Tarangire, Ngorongoro, Oldupai Gorge, Lake Manyara na kisha kuelekea Kijiji cha Butiama na kuzuru Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Hii ni kampeni ambayo kampuni ya Lakeland Africa imeianzisha kwa lengo la kuwawezesha Watanzania kuitembelea na kuijua nchi yao. Usafiri unautumika ni gari maalum linaloonekana ktk picha ya juu..

Hapa wakiwa kwenye moja ya majengo ya kale yaliyotumika wakati wa biashara ya watumwa huko Saadani.

Chef akiweka mambo sawa baada ya wadau kupiga kambi ndani ya hifadhi ya Saadani

 Wasafiri na kikosi kazi cha lakeland wakipumzika na kupata chai ya jioni ndani ya hifadhi ya taifa ya Saadani. Vifaa vyote vinabebwa na Lory hilo sambamba na wageni wenyewe.

Asubuhi kwenye campsite waliyolala wadau walioa ktk msafara huu

Gamedrive ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani. Ungana na Lakeland Africa Limited kwenye facebook ili uwe unapata updates na picha za safari ni nyinginezo moja kwa moja.

picha zote ni toka ktk ukuta wa facebook wa Lakeland Africa Limited.

No comments:

Post a Comment