Monday, December 17, 2012

Machweo ndani ya Selous Game Reserve

Ifikapo saa 12 kamili jioni, huo ndio unakuwa mwisho wa shughuli za mizunguko ndani ya hifadhi. hata kwa wewe mwenye kibali, kibali chako kinakuwa kinafika ukomo muda huo. Kimsingi unatakiwa uwe umeshatoka nje ya hifadhi au uwe umefika kwenye hoteli au campsite yako unayolala ndani ya Hifadhi. nje ya hapo ukikutwa unatangatanga porini mida hii unajiweka katika hali ya kukamatwa na kutozwa faini au kuchukuliwa hatua za kisheria.

 Asikwambie mtu, kuna raha ya kipekee kuwepo ndani ya hifadhi pale jua linapozama. Utasikia milio ya kila namna. kuanzia ya wanyama wakali mpaka ndege wadogo wadogo wakielekea kwenye viota vyao au wale wanaofanya shughuli zao jua linapozama. Kwakuwa hoteli na camp zilizo ndani ya hifadhi hazina uzio, nafasi ya wageni kutembelewa na wenyeji wao (wanyama wa porini) ni kubwa na huwa na hamasa ya namna ya kipekee japo tahadhari ni muhimu - inategema na mwenyeji anayewatembelea wageni wake.

Ni kutokana na hamasa hii unayoipata ukilala ndani ya hifadhi, ndio inayopelekea huduma za malazi ndani ya hifadhi kuatikana kwa bei ya juu. Hii inachangiwa na matozo ya ziada ambayo wamiliki wa hoteli zilizopo ndani ya hifadhi hulazimika kulipa. yote kwa yote, ukianza kwa kulala ndani ya hifadhi daima utapenda kila safari yako ufikie na kulala hoteli iliyopo ndani na sio nje.

Post hii ina picha za machweo ambazo tumezipata toka kwa Mdau Rajab wa Wildness Safaris. Hii ilikuwa ni camping safari ambapo Rajba na wageni wake walienda mbali kidogo kwa kuamua kulala kwenye mahema madogo kwenye moja ya public campsites ndani ya Selous Game Reserve. Walipata fursa ya kuliona jua likizama na hata kuwaona Twiga aka Warefu walioisogelea camp yao kwa ukaribu kabisa.


No comments:

Post a Comment