Sunday, December 16, 2012

Tented Camping - Wildness Safaris Tanzania

Tented camping ni moja ya namna ambayo mgeni anaweza kupata huduma ya malazi anapotembelea eneo au hifadhi hapa nchini na kwengineko duniani. Licha ya kuwa ni njia nafuu (kigharama) lakini pia  ni namna moja ambayo humweka mgeni karibu kabisa na mazingira na wanyama anaoenda kuwatembelea. Wakati mgeni anaweza kutozwa gharama isiyopungua $200 kwa usiku mmoja kwenye hoteli iliyopo ndani ya hifadhi lakini mgeni huyo huyo anweza kulala kwa gharama ya $10-$15 akiamua kufanya camping. Gharama hizi hutofautiana lakini hapa zimewekwa ili kukupa mwanga wa tofauti zilizopo.

 kwa campsite ambazo zipo nje ya maeneo ya hifadhi gharma ndio huwa ni ndogo zaiidi. baadhi hufikia mpaka $5 kwa usiku mmoja kwa mgeni mmoja. Changamoto anayokuwa nayo mgeni kuwa na vifaa vyake vya malazi na timu ya kumhudumia; Wapishi na wasaidizi wengineo. Kama unaanda safari yako na kampuni yenye uzoefu wa camping Safari, haya yote husimamiwa na kampuni na wewe unabaki kufurahia safari tu. Hizi ni picha za moja ya Camping Safari iliyokuwa inasimamiwa na Kampuni ya Wildness Safaris huko Mloka, nje kidogo ya pori la akiba la Selous. Jengo linaloonekana nyuma ni jengo mahususi kwa wapishi kuandalia maakuli ya wageni wao. Kimsingi ni jiko. Huduma nyingine binafsi zinakuwa zinapatikana kwenye jengo jingine.

 Baadhi ya mahema mgeni hulala kwenye godoro chini kama inavyoonekana kwenye picha hii

 Madirisha kwa ajili ya mzunguko wa hewa yanakuwepo pia

Hili hapa lina kitanda na godoro ndani.

Shukran ya picha zote kwa mdau Rajab wa Wildness Safaris Tanzania

No comments:

Post a Comment