Monday, December 31, 2012

Mandhari ya Matambwe - Selous Game reserve

Selous Game Reserve - Matambwe gate
Matambwe ni eneo ambako ndipo yalipo makao makuu ya wahifadhi na wasimamizi wa pori la akiba la Selous. Reli ya TAZARA nayo inakatisha katikati ya eneo hili ambako yapo makazi, ofisi za wahifadhi sambamba na geti la kuingilia ndani ya pori la akiba la Selous. Majengo unayoyaona ni sehemu ya majengo ya Ofisi, nyumba za maofisa wanyamapori wanaosimamia Selous na hata sehemu za kijamii kama vile social club, hospitali na maduka. yote haya yapo ndani ya eneo la hifadhi ambalo lina wanyama pori. Hili ndilo eneo ambalo lina uhakika wa kupatikana kwa Tembo kipindi kizima cha mwaka kwenye ukanda huu wa Matambwe.

Selous Game Reserve - Matambwe gate

Selous Game Reserve - Matambwe gate
Ni Kibanda kwa ajili ya wasafiri watakaokuwa wanasubiri treni kuendelea na safari. Treni za TAZARA husimama na kuchukua abiria wanaelekea mikoa ya kusini au maeneo mengine ya nchi inakopita reli ya TAZARA.

Selous Game Reserve - Matambwe gate

Selous Game Reserve - Matambwe gate
Mgeni anayeingilia geti la Matambwe ni yule aliyekuja kwa kupitia Morogoro, Matombo mpaka Kisaki. Matambwe haipo mbali na Kisaki. Umbali kati ya geti la Matambwe na Geti la Mtemere (Mloka, Rufiji) ni 80km. Geti la Mtemere lipo upande wa Rufiji ambako wanaingilia wageni waliopita barabara ya Kilwa/Mtwara. Umbali wa Kilometa 80 wote upo ndani ya pori la akiba la Selous. Na hii ni kwenye eneo lilitengwa maalum kwa safari za utalii wa picha, kama ambavyo wengi tunafanya. Maeneo na kanda nyingine zimetengwa kwa ajili ya vitalu vya uwindaji wa kitalii. Hapa Matambwe pia kuna uwanja mdogo wa ndege ambapo baadhi ya wageni wanaotumia ndege ndogo za abiria wanashukia hapo na kuanza safari zao ndani ya hifadhi. Hotel kadhaa zipo eneo hili baadhi zikiwa nje ya eneo la pori la akiba kama vile Sable Mountain Lodge au Ndovu Lodge (Kisaki). Geti la Matambwe lipo mkoa wa Morogoro.

Selous Game Reserve - Matambwe gate


Selous Game Reserve - Matambwe gate

Selous Game Reserve - Matambwe gate

No comments:

Post a Comment