Thursday, November 15, 2012

Bwawa la viboko Mikumi NP

Mikumi National Park
Limezoeleka zaidi kama Bwawa la Viboko la Mikumu lakini ndani ya bwawa hili kuna zaidi ya viboko. Mamba nao wanapatikana kama jinsi ambavyo 'bango' linavyoonyesha na picha zinazofuata. Hapa wageni wanaruhusiwa kushuka kwenye magari yao na kujinyoosha. pia ni sehemu ya kupatia maakuli japo hakuna meza. Kwa ajili ya kupata maakuli wageni watalazimika kula chakula chao kwenye magari.   

 
Mikumi National Park
Bango liliopo pembeni ya Bwawa hili likitoa maelekezo ya muhimu kwa wageni na mambo ya kuzingatia wanapokuwepo hapo. Usafi ni moja ya mambo ya msingi ambayo mgeni anapaswa kuyazingatia anapokuwepo hapa na sehemu nyingineza ndani ya hifadhi.

Mikumi National Park
 Hawa jamaa ndio wanyama wa porini ambao wanaoongoza kwa kuuwa watu wengi barani Africa (Sub Sahara Africa). Kikubwa ni ukali wao ktk kulinda himaya zao ambazo zipo kwenye mito. Wengi wanaokumbwa na mikasa ya hawa majamaa ni wavuvi au watu wanaoenda kwenye mito na mabwawa kwa shughuli za kuchota maji au kufua

Mikumi National Park
 Porini wamepewa jina la Mkasi.

Mikumi National Park
 Huyu alikuwa nje ya bwawa akiota jua ili apandishe joto la mwili asiwe goigoi. Hawa ni wanyama wenye damu baridi, hutegemea joto linalopatikana kwenye mazingira ili walitumie kupandisha hali ya joto la miili yao. Wasipofanya hivyo huwa magoigoi hali ambayo huwaweka ktk wakati mgumu wa kujitafutia chakula.

Mikumi National Park
 Unaweza kupata uwiano wa ukubwa wake wa mwili sambamba na mazingira aliyopo. Bwawa linaonekana dogo lakini mamba wanaoishi humo ni wakubwa vya kutosha.

Mikumi hippo Pool
Ni ndiga ya Mdau Rajab wa Wildness Safaris Tanzania aliyekuwa huko mikumi hivi karibuni na kuturushia picha.

No comments:

Post a Comment