Shughuli yake kubwa inayompa ugali wake ni kuongoza wageni kwenye safari za matembezi. Mwenyewe hujigamba kwa kuziita true Africa walking safari. Daima anapokuwa mzigoni huwa anavaa mavazi ya asili kabisa ambayo kayatengeneza kwa magome ya miti huku akiwa amebeba ngao, mkuki na kikapu chake cha kuobebea mitishamba.
Safari zake huwa zinafuata barabara na wakati mwingine huacha barabara na kuingie mapori. yeye huzunguka na wageni wake nje ya hifadhi japo pia wanyama wa porini (wakali na wapole) wanakuwepo. Kwa ajili ya tahadhari na usalama, anapofanya safari za miguu na wageni wake daima huwa anaambatana na askari toka kwenye campsite waliofikia wageni wake ambaye huwa na bunduki kwa ajili ya tahadhari. Angalia picha ya pila juu, upande wako wa kushoto utamuona askari mwenye riffle. Elewa ya kwamba safari za matembezi ndani ya hifadhi, mgeni husindikizwa na Ranger wa Maliasili na guide wake au ranger peke yake. Drogba yeye anacheza nje ya hifadhi.
Safari zake huwa na vituo vingi ndani yake na kwenye kila kituo kuna jambo ambalo huona ni vyema wageni wake wapate kulifahamu. wakati mwingine mkiwa nae safarini mnaweza kukutana na wanyama na wakati mwingine safari zake zikawa ni mafunzo ya wanyama na mazingira yao zaidi.
Mgeni hufundishwa namna ya kutambua nyayo za wanyama mbalimbali ambazo huwa wanakutana nazo wakiwa safarini.
Safari ikiendelea na vituo vikiwemo ndani yake
Ahsante ya picha Mdau Rajab - Wildness Safaris Tanzania
No comments:
Post a Comment