Thursday, November 15, 2012

Gharama za Kutalii Gombe kwa raia wa Afrika Mashariki

Gharama halisi kwa mtalii yeyote wa ndani awe Mtanzania au raia nchi zinazounda Afrika Mashariki:

Kutoka Kigoma mjini kwenda Hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa usafiri wa boti ya abiria ni Tsh. 4,000
Kuanzia Gombe kurudi mjini ni Tsh. 4,000.
Usafiri huu unapatikana siku zote isipokuwa Jumapili tu.
Muda wa boti kuondoka ni saa 6:00 (saa sita kamili mchana).
Ni usafiri salama tofauti na watu wanavyofikiria.
Ukifika Gombe wafahamishe kuwa nashukia Kasekela ( special area for tourism activities).
Hakuna usafiri wa kwenda na kurudi siku hiyo hiyo isipokuwa kwa ukodi boti binafsi ambazo ni gharama zaidi.

Ukifika Gombe utalipia TSh. 1500 kama  kiingilio (entrance fee) na TSh. 500 kama fedha ya kutembea (trekking fee) kwa siku moja. Utapata huduma ya malazi kwa kulipia kwa kichwa na si chumba, yaani mtu mmoja atalipia TSh. 5,000 tu kwa usiku mmoja, kama mpo wawili na mkatumia chumba kimoja mtalipia TSh. 10,000 tu kwa usiku mmoja pia. Gharama ya chakula ni TSh. 5,000 kwa mlo mmoja. Gharama ya vinywaji ni TSh. 1,500 kwa soda na 2,500 kwa bia.

Kumbuka: Unakuja Gombe kwa boti ya abiria, utafika mchana, siku inayofuata utafanya utalii na siku ya tatu utapanda boti hilo linalopita Gombe saa moja kamili ya asubuhi. Hivyo ni vizuri ujiandae kwa malipo ya nights 2 na milo ya siku 2. Kwa mtu asiye na mambo ya luxury sana akijipanga na TSh. 50,000 tu itatosha na chenji itarudi.

Watoto chini ya miaka 15 hawaruhusiwi kwenda kutalii bali watabaki rest house kwa usalama wa kutosha.

KARIBUNI SANA ndugu!

No comments:

Post a Comment