Friday, October 5, 2012

Kenge na Simba - Selous GR


Hii ilitokea ktk eneo pembeni ya Ziwa Nzelekela huko ndani ya pori la akiba la Selous. Kenge anayeonekana alikuwa kajificha kwenye hicho kichaka. akawa anatoka kwenye kichaka ili aelekee ziwani. baada ya kutoka nje ya hicho kichaka, alibaini ya kwamba amechomozea sehemu iliyokuwa ina simba jike wawili. Kwa kugundua hatari iliyo mbele yake, Kenge huyu aliamua kutulia tuli akisikilizia kama sharubu hao wangemletea shida au wangeachana nae. Mwisho wa siku sharubu hao waliamua kuachana na kenge huyo na kuendelea kuuchapa usingizi wao.
Video imetoka ktk maktaba ya Tembea Tz blog

No comments:

Post a Comment