Wednesday, October 3, 2012

Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.

this photo from tanzaniaparks.com
 Ni moja ya hifadhi za taifa ambazo ni kama hazimu lakini zipo. Ipo mkoani Kilimanjaro, katika wilaya ya Same. Ni moja ya hifadhi za hapa nchini ambako Mbwa mwitu pamoja na vifaru wanatunzwa kwa lengo la kuzaliana ili kuweza kurudisha idadi yao ktk mapori na hifadhi nyingine hapa nchini. Awali ilikuwa ni pori la akiba mpaka miaka ya hivi karibuni ilipopandishwa hadhi na kuwa hifadhi ya taifa. Ni Hifadhi yenye mkusanyiko wa wanyama wengi utakaowategemea kuwakuta kwenye hifadhi nyinginezo. Kitu kimoja cha kipekee kwa Mkomazi ni kwamba hutumika kama kituo kwa ndege ambao huhama kati ya bara Ulaya na Afrika. Ni hifadhi ambayo huwavutia sana wageni wanaopenda kuangalia aina mbali mbali za ndege. Ndege wanaohama hutumia maeneo ya hifadhi kama vituo vyao vya kupumzikia wakiwa wanaelekea kusini mwa Afrika au kipindi wanapokuwa wanarudi makwao - Bara la Ulaya.

Picha juu ni moja ya njia zinaweza kukufikisha kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi. Hii njia ipo  katika barabara kuu ya Arusha-Dar. Njia nyingine inayoweza kukufikisha Mkomazi ni ile inayoingilia pale Same "mjini". Hii ipo karibu na geti kwani inaelezwa ya kwamba ni mwendo usiozidi Kilometa 10 tokea h Same, unakuwa tayari ndani ya eneo la hifadhi. Hiyo ya kwenye picha juu ni umbali wa kilomenta 66 kama zinavyoonekana ktk bango. Njia hii imezoeleka na wengi kama njia ya kwenda Gonja. Kwa anayetumia njia hii ataingilia geti lijulikanalo kama Njiro. Kwa yule atakayeingilia njia ya Same ataingia ktk hifadhi kupitia geti la Zange.

Njia kuu ya DSM - Arusha ikionekana huku njia panda ya kuelekea Gonja hadi hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ikionekana. Milima inayoonekana kwa nyuma ni safu ya Milima ya Usambara.


View Larger Map
Picha toka mkataba ya Tembeatz na Ramani toka Google Maps.

Unaweza kupata taarifa zaidi kupitia http://www.tanzaniaparks.com/mkomazi.html

No comments:

Post a Comment