Tuesday, October 9, 2012

Jokofu la Chui - Akiba haiozi - Selous GR

Wildness Safari Tanzania Selous
 Haikuweza kufahamika mara moja mnyama aliyeuwawa na kuning'inizwa mtini kwa namna hii lakini ni dhahiri mnyama anayehusika kwa uhifadhi wa akiba Kwa style hii ni Chui aka wa juu. Katika familia ya paka wawindaji, chui huhifadhi mawindo yake juu ya mti ambako wanyama wenzake hawawezi kuYAfikia kirahisi na kumpokonya windo lake. Style hii humwezesha chui kujihakikishia mlo na pia kukwepa adha ya kula chakula kwa mkupuo na haraka kwa kuwa ana uhakika na friji lake halivamiwi kirahisi. Ukiangalia vyema utabaini ya kwamba ameenda kuuficha huo mzoga wake kwenye matawi madogo. kwa hapo alipoweka, hata wale ndege wa mizogo Tai (tumbusi) hawewezi kuufikia kwani anakuwa anazuiwa na matawi. Kumbuka ya kwamba Tumbusi ni moja ya ndege wakubwa wanaopatikana kwenye mapori na hivi huhitaji sehemu ya wazi kuweza kutua na kuruka.

Wildness Safari Tanzania - Selous
Chui ni mnyama ambae hujenga na kulinda himaya yake.Kwenye himaya ya chui mmoja (dume) si rahisi kukuta chui mwingine ambaye hana uhusiano na mwenye kaya (territory). Na wao pekee ndio wenye uwezo mzuri wa kukwea miti hata ile iliyonyanyuka wima na kuweza kufika kule kwenye fito nyembamba. Akiweka huku basi ana uhakika wa kukuta windo lake likiwa salama. kama kuliwa basi litakuwa limeliwa na jamaa au ndugu yake. Chui mmoja akiingia kwenye kaya ya mwenzie hufukuzwa kama mbwa mwizi na mara nyingi akibisha hutembezewa kichapo kikali.
(picha toka kwa - Wildness Safaris Tanzania)

No comments:

Post a Comment