Tuesday, June 12, 2012

Zifahamu namba za kuripoti matukio au mipango ya ujangili

Wizara ya Maliasili na Utalii inawaomba wananchi na watu wote wenye nia njema kushirikiana na Serikali katika kupambana na ujangili na uvunaji haramu wa mazao ya maliasili kwa kuwafichua wahalifu.

Wizara inawapongeza wananchi wote ambao wamekuwa wakitoa taarifa zilizowezesha majangili au wavunaji haramu kukamatwa wakiwa na mazao waliojipatia kinyume cha sheria.

Wananchi wanaombwa kuendelea kutoa taarifa katika ofisi yoyote ya Maliasili au Polisi au kwa kutumia namba za simu 0784 883388 na 0714 250050.

Maliasili ni ya wananchi wote, tushirikiane kuilinda kwa manufaa ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.

KATIBU MKUU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
7 June 2012

No comments:

Post a Comment