Thursday, June 7, 2012

Umewahi kuona hema la ghorofa?


Kama hujawahi (kama mimi) basi utakuwa umepata sababu moja ya ziada ya kukufanya utembelee maonesho ya Karibu Fair 2012 pale Mkoani Arusha ktk Viwanja vya Magereza (karibu na Arusha Airport). Hili ni hema ambalo linatumika kwa shughuli za malazi kwa wageni wanapokuwa porini. Hususan wale wageni ambao hupenda kufanya camping na kuachana na kulala kwenye mahoteli. Moja ya makampuni yanayoshiriki Karibu Fair mwaka huu imeamua kuja kuwaonyesha wageni na wadau bidhaa hii. Ni Hema la kipeke kwani linahamishika.

No comments:

Post a Comment