Thursday, June 7, 2012

Karibu Fair 2012 kuanza Kesho Arusha


Karibu Fair Arusha
Na maandalizi ndiyo yanazidi kupamba moto ndani ya viwanja vya Magereza, nje kidogo ya jiji la Arusha. Maonesho haya yanawaleta wadau mbalimbali ktk sekta ya utalii toka pande nyingi za duniani kuja kunadi kazi wananzozifanya na bidhaa wanazouza. Maonesho haya yanataraji kuanza Kesho ambapo TembeaTz imetonywa ya kwamba kama hakutakuwa na mabadiliko, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Balozi Hamis Kagasheki atakata utepe kesho asubuhi na kuyazindua rasmi maonesho haya. Hadi jana wakati picha hizi zikipigwa, makampuni mbalimbali yalikuwa tayari yameshaanza kuweka nakshi na mapambo sehemu zao za kunadi kazi zao.

Karibu Fair Arusha
Baadhi ya mafundi na wafanyakazi toka kampuni mbalimbali za utalii wakiendelea na kazi ya kufunga mahema na vifaa mbalimbali vya kazi ambavyo vitakuwa vikionyeshwa kwa wageni watakaotembealea Maonesho ya Karibu fair huko Arusha kuanzia kesho mpaka siku ya Jumapili 10-06-2012.

Karibu Fair Arusha
 Kazi inazidi kuendelea.

Karibu Fair Arusha
 Ulinzi upo kamili gado

Karibu Fair Arusha
 Biashara asubuhi, jioni mahesabu....

Karibu Fair Arusha
Sehemu mbalimbali za miji ya Arusha na Moshi imepambwa kwa mabango yanayowataarifu wageni na wenyeji kuhusu maonesho haya ambayo ni ya kipekee katika ukanda wa Afrika mashariki.


Karibu Fair Arusha
Tayari baadhi ya huduma za kiofisi za Karibu fair zimeanza kutolewa uwanja wa maonesho ili kurahisisha huduma na kuratibu mambo kwa karibu. Wafanyakazi wa Karibu Travel & Tourism fai wakiwa mzigoni kuhudumi wateja wao ktk viwanja vya Magereza huko Arusha.


Karibu Fair Arusha
Wengine wameshafunga minara yao ya mawasiliano ya Internet ili waweze kuwahudumia wateja watakaowatembelea papo hapo kwenye uwanja wa maonesho. 

Picha zote hizi zilipigwa jana na kwa taarifa ambazo blog yenu ya TembeaTz imezipata toka Arusha zinasema ya kwamba siku ya kazi imezidi kupanga moto huku kila mshirikia akihakikisha anakamilisha maandalizi ya eneo lake mapema na kikamilifu. Unaweza kujua ratiba kamili ya maonesho haya kwa kubofya hapa. Kiingilio ni Sh 3000 kwa ticket ya siku nzima. (Shukran kwa Timu ya Karibu Fair kwa mkusanyiko wa picha hizi)

No comments:

Post a Comment