Friday, June 8, 2012

Karibu Fair Kuanza rasmi Leo Arusha

Ni Katika viwanja vya magereza nje kidogo ya jiji la Arusha, njia ya kuelekea Babati, Ngorongoro, Dodoma. Mamia ya wadau mbalimbali toka ndani na nje ya nchi na bara letu wanashiriki maonesho ya mwaka huu.

Wageni wameanza kutembelea mabanda huku baadhi ya washiriki wakimalizia maandalizi ya dakika za mwisho kabla uzinduzi rasmi haujaanza.

 Kila mtu anashughulika kuhakikisha sehemu yake ipo sawa saawa.
Makampuni yanayouza magari sambamba na yale yanafanyia marekebisho magari yanayotumika katika sekta ya Utalii yameshiriki pia. Mwaka huu mengi yamekuja kikamilifu kwa lengo la kunadi kazi zao na kuweza kupata wateja wapya au kukutana na wateja wa siku zote.

Taasisi mbalimbali za Serikali zinahusika na sekta ya Utalii zinashiriki na banda unaloliona ni banda ambalo wote kwa pamoja wapo hapo ili kuweza kutoa taarifa na kunadi kazi zao kwa watakaowatembelea.


Tembea Tanzania Blog imeshatia maguu kwenye viwanja hivi na tutaendelea kukuletea habari mbalimbali ambazo tutazikusanya hapa kwenye maonesho haya ya mwaka huu.

No comments:

Post a Comment