Moja ya ndinga za safari za kampuni ya RA Safaris zikivuja moja ya mito inayopeleka maji kwenye Ziwa Natron huko mkoani Arusha. Kwa mbali ni Mlima wa Oldonyo Le Ngai ambao ni moja ya milima ya volcano ambayo volcano yake bado haijatulia. Ni miaka michache iliyopita mlima huu ulionyesha dalili za kulipuka hali iliyopelekea wakazi wa maeneo karibu na mlima kuhamishwa. Ukiachana na hayo, Eneo lilipo mlima huu ni eneo zuri kwa mapumziko na kuna campsite nyingi na nyingine zikiwa pembezoni mwa Ziwa Natron. Ziwa Natron halipo mbali na ilipopigwa picha hii. Shukran kwa Mdau Gideon wa RA Safaris kwa picha na dondoo muhimu.
No comments:
Post a Comment