Tuesday, June 5, 2012

Taswira Za Serengeti NP toka RA Safaris

Hapa ni Ndani ya Serengeti eneo lijulikanalo kam Moru Kopjes (inatamkwa Copies) ambako kikosi kazi cha RA safaris kiliikuta Migration ya Nyumbu na wanyama wengine ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti. Hii ilikuwa ni mwaka jana. Taswira hii imepigwa tokea Moru Kopjes.

wageni waliokuwa wametembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakipata mlo wa mchana juu ya moja ya majabali ya mawe yaliyopo ndani ya hifadhi. Majabali haya hujulikana kama Kopjes. Kopjes ni neno la kiholanzi lenye kumaanisha kichwa kidogo. Haya majabali yanakuwa na majina tofauti tofauti. Kule maeneo pembezoni na ziwa Victoria yanajulikana kama Bismarck. Majabali unayoaona baada ya magari ni moja ya Kopjes ambazo zipo ndani ya Serengeti. Ni moja ya vivutio vikubwa kwa wageni kwenye hifadhi hii.

Mawio ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti; 

Wapenzi wa taswira za Mawio, Zawadi yenu hiyo toka RA Safaris. Shukran kwa timu nzima ya RA Safaris kwa ushirikiano wenu mnaonyesha kila siku na blog ya Tembea Tanzania.

No comments:

Post a Comment